LOADING...

+255 222215701   info@mloganzila.or.tzMuhimbili yatakiwa kuimarisha utafiti na uvumbuzi

Mar 15 2019

Wataalam wa afya nchini wametakiwa kujikita zaidi katika kufanya utafiti na uvumbuzi ili kuleta matokeo chanya katika utoaji wa huduma za afya.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Charles Majinge wakati akifungua kongamano la kwanza la kisayansi kuhusu kutafsiri tafiti kwa vitendo katika kutoa huduma za tiba lililofanyika Hospitali ya Mloganzila.