
Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga&Mloganzila) imeshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Shirikisho la Dunia la Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (WFNS), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo, tarehe 16 Aprili 2026.
Akizungumza wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipotembelea banda la hospitali hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Delilah Kimambo, ameeleza kuwa hospitali hiyo ipo mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora wanapofika hospitalini hapo.







