Muhimbili National Hospital – Mloganzila

WATAALAMU WAJADILI NAMNA YA KUBORESHA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO, KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI

Wataalamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na Hospitali ya Wilaya ya Kinondoni wamekutana kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu namna ya kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto kwa lengo la kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.

Changamoto zilizobainishwa ni pamoja na mama kuchelewa kufika hospitalini, kutotambua dalili za hatari, kutofuata maelekezo ya wataalamu wa afya pamoja na changamoto za usafiri wa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya kibingwa.

Mkuu wa Idara ya Mama na Mtoto Muhimbili-Mloganzila, Mwanaheri Chubi, amesema Mloganzila iko tayari kuendelea kushirikiana na hospitali nyingine ili kuongeza ujuzi wa watoa huduma na kuimarisha huduma za mama na mtoto. @muhimbili_taifa @wizara_afyatz @elimu_ya_afya

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

MNH - Mloganzila: Premier Clinic Online Appointment
Book your medical appointments online. Skip the long queues and book your appointment with our specialists from the comfort of your home.
Scroll to Top