LOADING...

+255 222215701   info@mloganzila.or.tzWaziri Ummy aipongeza Mloganzila, awaagiza wataalam kuandaa takwimu za kitaifa

Mar 3 2019

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amewaagiza watalaam wa wizara ya afya kuhakikisha kunakuwa na takwimu za kitaifa kuhusu hali ya usikivu nchini ili kubaini ukubwa wa tatizo hilo.
Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam alipokua akizungumza katika maadhimisho ya siku ya usikivu duniani ambapo katika kuadhimisha siku hiyo Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imetoa huduma ya upimaji wa usikivu bure kuanzia Machi 02 hadi Machi 03, 2019.

Amesisitiza kuwa takwimu hizo zigawanywe kwa watu wazima na watoto wenye umri wa kwenda shule ili kuisaidia Serikali kuweka afua na kuona ni jinsi gani itawawezesha watoto hao kufanya vizuri katika masomo yao.